Friday, June 3, 2016

KLABU 2 ZA MISRI VITANI KUWANIA SAINI YA DONALD NGOMA

Klabu za Misri Al Ahly na Zamalek zipo katika vita ya kuwania saini ya Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma.




Uwezo mkubwa wa Donald Ngoma anapokuwa uwanjani umezifanya klabu nyingi kuhitaji saini ya mchezaji huyo anaeitumikia klabu ya Yanga kwa sasa. Ngoma amekuwa katika kiwango bora na ameisaidia timu yake ya Yanga kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Vodacom, FA Cup pamoja na kufika hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Africa.

Klabu za Misri, Zamalek na Al Ahly zimeonyesha nia ya kumnasa mshambuliaji huyo kutokana na kuvutiwa na uwezo wake.

Ngoma kwa sasa amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake wa kuitumikia Yanga na ripoti zinasema Mshambuliaji huyo ameshaanza mazungumzo na Al Ahly huku Zamalek nao wakiingia katika vita hiyo.
Lakini licha ya tetesi hizo, Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amesema hawajapokea maombi kutoka katika klabu yoyote yanayoonyesha kumuhitaji Ngoma.

"Tunasikia taarifa hizo kupitia kwenye mitandao mbalimbali na vyombo vya habari lakini rasmi hatujapokea barua kutoka klabu yoyote inayomzungumzia Ngoma, ikitokea tutakaa kama uongozi na bechi la ufundi kujadili kama tumuuze au vinginevyo" alisema Sanga alipozungumza na Goal.

Ngoma amefunga jumla ya magoli 21 katika mashindano yote msimu huu, 17 kati ya hayo akifunga katika ligi kuu Vodacom.

0 comments:

Post a Comment