Tite |
Tite 55, anachukua nfasi ya Dunga aliyetimuliwa mara baada ya Brazil kutolewa hatua ya makundi katika michuano ya Copa America inayoendelea huko nchini Marekani. Peru ndo iliwafungisha virago Brazil baada ya kuwafunga goli 1 - 0 katika mchezo ambao Brazil walikuwa wanahitaji sare yoyote wasonge mbele.
Licha ya ukweli kwamba katika mchezo wa soka kila kitu kinawezekana lakini ukiangalia katika viwango vya Fifa katika ubora wa soka Brazil inashika nafasi ya 7 wakati Peru ipo nafasi ya 148, hivyo kuonyesha wazi kuwa Brazil walikuwa katika kiwango kibovu.
"Tite hafanyi tena kazi na Corinthians. Amekubali mwaliko uliotolewa na shirikisho la mpira wa miguu Brazil (Brazilian Football Confederation-CBF)" alisema Rais wa Corinthians Roberto De Andrade.
Dunga aliichukua Brazil kutoka katika mikono ya Felipe Scolari mwaka 2014. Brazil iliachana na kocha huyo wa Zamani wa Chelsea baada ya fedheha kubwa waliyoipata katika michuano ya kombe la dunia walipokubali kipigo cha magoli 7 - 1 kutoka kwa Ujerumani.
Dunga, Nahodha aliyeiwezesha Brazil kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia mwaka 1994, awali aliifundisha Brazil kuanzaia mwaka 2006/10 na kufanikiwa kushinda kombe la America (Copa America) mwaka 2007 na kombe la mabara mwaka 2009, kabla hajatimuliwa tena baada ya michuano ya kombe la Dunia mwaka 2010 na kuja kuichukua tena Brazil baada ya Scolari kuachia ngazi.
0 comments:
Post a Comment