Wednesday, June 8, 2016

STEPHEN KESHI AFARIKI DUNIA

Mchezaji wa zamani wa Nigeria na baadaye akaja kuwa kocha wa Timu hiyo ya Super Eagles Stephen Okechukwu Chinedu Keshi ameiaga Dunia saa chache zilizopita.



Watu wake wa karibu wanasema hakuwa na tatizo lolote la afya lakini inadhaniwa amepatwa mshituko wa moyo.
Mwishoni mwa mwaka uliopita Keshi alimpoteza mkewe kutokana na saratani, nduguze wanasema huenda ameshindwa kuibeba hali hiyo ya kumkosa mkewe waliyedumu naye kwa miaka 35.


CHANZO: BBC

0 comments:

Post a Comment