Thursday, June 23, 2016

ANTOINE GRIEZMANN AONGEZA MKATABA ATLETICO

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya na klabu ya Atletico Madrid utakaomuweka klabuni hapo hadi 2021.

Griezmann alikuwa akihusishwa na kujiunga na vilabu vya ligi kuu ya Uingereza lakini mwenyewe amesema anafurahia maisha ya Atletico.

Baada ya kusaini mkataba huo wa miaka mitano Griezmann alisema amefarijika kuendelea kuwa sehemu ya Atletico na kwamba atajitahidi kujituma ili kiwango chake kiwe kinapanda mwaka hadi mwaka.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment