Ngassa ambaye yupo likizo kwa sasa amesema Yanga walicheza vizuri sana katika mchezo huo huku akisema kilichowaangusha ni kushindwa kuzitumia nafasi nyingi za magoli walizozitengeneza kwenye mchezo huo.
"Walicheza vizuri sana na walitengeneza nafasi nyingi lakini kwa bahati mbaya tu walishindwa kuzitumia nafasi hizo kufunga magoli. Walipambana hadi dakika za mwisho wakitaka kusawazisha goli hilo, kilikuwa ni kiwango kizuri sana." alisema Ngassa mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga.
Yanga sasa ina kibarua kizito dhidi ya TP Mazembe mchezo utakaopigwa Jijini Daresalaam Juni 28, 2016.
0 comments:
Post a Comment