Saturday, May 7, 2016

CAMEROON YAPATA PIGO, MUNGINE AFARIKI UWANJANI


Kiungo wa timu ya Taifa ya Cameroon na klabu ya Dinamo Bucharest, Patrick Ekeng amefikwa na mauti muda mchache mara baada ya kudondoka uwanjani wakati akiitumikia klabu yake katika mchezo dhidi ya klabu ya Viitorul Constanta.

Patrick Ekeng alidumu uwanjani kwa dakika saba tu mara baada ya kuingia katika kipindi cha pili akitokea benchi. Wakati akiwa mchezoni alidondoka na kubaki akiwa amelala katika dakika ya 70.Timu yake inayoshiriki katika ligi kuu ya Romania, RomanianLiga  ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-2 katika mchezo ambao ulikuwa ukioneshwa moja kwa moja huko Romania. Chombo kimoja cha habari kimeripoti kwamba alipatwa na shambulio la moyo.

Mara baada ya tukio hilo kutokea alichukuliwa kwa haraka na gari la kubeba wagonjwa na kuwahishwa katika hositali iliyokuwepo karibu na uwanja lakini dakika chache baadae alifikwa na mauti.Alijiunga na klabu hiyo mwezi January na mchezo wa usiku wa jana ulikuwa ni mchezo wake wa saba. Kabla ya kutua Dinamo Bucharest alishawahi kutumikia klabu kadhaa barani Ulaya zikiwemo Le Mans, Lausanne, na Córdoba.
Kwa upande wa timu ya Taifa ameshakitumikia kikosi cha wakubwa cha Cameroon mara saba.

Cameroon ina kumbu kumbu ya kumpoteza nyota wake Marc-Vivian Foe ambae alifikwa na mauti june 2003 akiwa anaitumikia timu yake ya Taifa ya Cameroon katika mchezo dhidi ya Colombia katika FIFA Confederations Cup hatua ya nusu fainali kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Stade de Gerland.
Alidondoka katika dakika ya 72 ya mchezo, madaktari walijitahidi kuushtua moyo wake kwa dakika 45 lakini juhudi zao ziligonga mwamba.

TAZAMA JINSI HALI ILIVYOTOKEA UWANJANI HAPO



Source: Katanga Official Site


0 comments:

Post a Comment