Friday, May 6, 2016

LUIS SUAREZ ATUMA UJUMBE HUU KWA LIVERPOOL


Kufuatia ushindi wa 3 - 0, walioupata Liverpool jana dhidi ya Villarreal katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya kombe la Europa League, Mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ya Liverpool Luis Suarez amewatumia ujumbe wa pongezi wachezaji wa Liverpool aliowaita kuwa ni marafiki zake, Martin Skrtel na Philipo Coutinho.
Katika ujumbe huyo aliouandika katika akaunti yake ya twitter Suarez amesema “Hongereni Liverpool kwa kuingia katika hatua ya Fainali. Hongereni pia rafiki zangu Martin Skrtel na Philipo Coutinho”

Suarez alijiunga na Barcelona akitokea katika klabu ya Liverpool ambako alicheza kwa mafanikio makubwa.

Liverpool itacheza na Sevilla katika fainali hiyo  May 18 huko nchini Switzerland.

0 comments:

Post a Comment