Thursday, April 14, 2016

Tetesi Mpya Za Usajili Barani Ulaya Leo Alhamisi April 14,2016


Arsenal  Yamfukuzia Brozovic
Klabu ya Intermilan italazimika kumuuza nyota wake Marcelo Brozovic kwa ada ya Paundi Milioni 25 endapo itashindwa kufuzu kushiriki Michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya Msimu Ujao. Arsenal imeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.

Source: Tuttosport

Thursday, April 14, 2016 02:16


Ibrahimovic Huenda Akaenda Qatar
Zlatan Ibrahimovic anaweza kuendelea kubaki Paris-Saint German kwa misimu mingine zaidi kabla hajaamua kukubali ofa nono ya kwenda kucheza soka nchini Qatar na kutupilia mbali Vilabu vya Ligi Kuu Uingereza vinavyomtolea macho.

Source: Sport

Thursday, April 14, 2016 02:13

West Brom Inamtaka Sakho Kuziba Pengo La Berahino
Klabu ya West Brom inataka kumsainisha Straika wa West Ham United Diafra Sakho kuchukua nafasi ya Saido Berahino ambae yupo mbioni kuondoka klabuni hapo. Sakho kapoteza nafasi yake West Ham ambao wanataka kumsainisha Jordan Ayew, Christian Benteke au Wilfred Bony.

Source: The Sun

Thursday, April 14, 2016 01:36

Man Utd Kuingia Katika Vita Na PSG Kumgombea Mourihno
Klabu ya Manchester United itapanda ushindani mkubwa kutoka kwa Matajiri wa Ufaransa Paris-Saint German kama PSG wataamua kumfukuza Kocha wao Laurent Blanc kufuatia kuondolewa kwao katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Source: Daily Telegraph

Thursday, April 14, 2016 01:35

Juventus Inamwangalia Kwa Karibu Mshambuliaji Wa Liverpool Divock Origi
Klabu ya nchini Italia Juventus inaangalia uwezekano wa kumsajili Origi kutoka Liverpool  sambamba na Christian Benteke.

Source: Calciomercato.com

Wednesday, April 13, 2016 16:42

Oxlade-Chamberlain Ndio Chaguo Namba 1 La Southamton
Klabu ya Southampton inamwona Chamberlain kuwa ndo chaguo lao la kwanza, wamejiandaa kumfanya mchezaji huyo kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi  sambamba na kumpa ukapteni.

Source: Daily Mirror

Wednesday, April 13, 2016 01:51

Bale kutua Man Utd au Man City
Klabu ya Real Madrid ipo mbioni kumwongezea mkataba mnono Gareth Bale lakini mawakala wake wanafikiria kumrudisha Mchezaji huyo katika Ligi Kuu ya Nchini Uingereza Kujiunga Aidha na Manchester United au Manchester City.


Source: Tuttomercatoweb.com
Wednesday, April 13, 2016 01:46

0 comments:

Post a Comment