Klabu ya Liverpool imethibitisha kuwa beki wao Mamadou Sakho hatajumuishwa katika kikosi hicho baada ya uchunguzi uliofanywa na Uefa kugundulika kuwa alitumia dawa zilizokatazwa kwa wachezaji.
Sakho alipimwa baada ya mechi yao na Machester United iliyopigwa Old Trafford March 17 mwaka huu na majibu yakaonyesha alitumia dawa ambazo zimekatazwa kutumiwa na wanamichezo.
Sakho ameambiwa hadi kufikia Jumanne wiki hii awe amejibu tuhuma hizo.
Klabu ya Liverpool imesema haijazuiliwa kumtumia Sakho kwa sasa isipokuwa wao kama klabu imeona kwa kipindi hiki ambacho hili suala linafuatiliwa sio busara kwa wao kumtumia katika mechi zao.
Sakho mwenye miaka 26 anaweza kupata adhabu kubwa ya kufungiwa kucheza endapo vipimo ambavyo vitachukuliwa tena hivi karibuni vitarudisha majibu sawa na yale ya mwazo.
Beki mwenzie Kolo Toure aliwahi kufungiwa miezi 6 baada ya shirikisho la mpira nchini Uingereza kumtia hatiani kwa kosa la kutumia dawa za kupunguza unene (diet Pills) ambazo haziruhusiwi kwa wachezaji, Toure alitumikia adhabu hiyo akiwa na klabu ya Machester City mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment