Sunday, April 24, 2016

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya Leo Jumapili April 24, 2016


Barcelona imeandaa Paundi milioni 15 kumnasa Golikipa wa Leicester City
Barcelona inataka kumsainisha mlinda mlango wa Leicester City Kasper Schemeichel kuchukua nafasi ya Marc-Andre ter Stegen. Mabingwa hao wa Ulaya wameandaa kitita cha paundi milioni 15.

Van Gaal Amwekea Vikwazo  Memphis
Kocha wa Man Utd Louis Van Gaal ameweka vikwazo juu ya kumuuza mshambuliaji wake Memphis Depay. Depay ambae ana mwaka mmoja tu tangu ajiunge na klabu hiyo anatakiwa na vilabu vingi vya ulaya.

Tottenham wanaongoza mbio za kumfukuzia Lacazette
Tottenham wanazidi kumfukuzia kwa karibu straika wa Lyon Alexandre Lacazette lakini Manchester United, Everton na Liverpool nao pia wanamuhitaji mchezaji huyo mwenye thamani ya paundi million 23.5

Arsenal na Juve Zamgombea Ibrahimovic Mpya
Arsenal na Juventus wameingia vitani kupigania saini ya kinda anaefananishwa na Zlatan Ibrahimovic kutokana na umbile lake la urefu unaofikia futi 6’3”. Kinda huyo mwenye miaka 16 Dusan Vlahovic anachezea klabu ya Partizan Belgrade.

0 comments:

Post a Comment