Klabu ya Yanga imemwongeza mkataba wa miaka miwili beki wake wa kulia,Juma Abdul, Mkataba ambao utamuweka Mchezaji huyo klabuni hapo hadi Mei 2018.
kwa mujibu wa Meneja wa klabu ya Yanga Hafidhi Salehe ni kwamba Juma Abdul alisaini mkataba huo wa miaka miwili kabla hajaenda Misri kucheza na Al Ahly.
“Ni kweli Juma ameongeza mkataba mpya na ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga hadi mwaka 2018, na hakuna kingine kilicho tushawishi kuongeza mkataba naye zaidi ya mchango wake katika timu msimu huu,”alisema Salehe
0 comments:
Post a Comment