Tuesday, April 12, 2016
Hizi Ndio Tetesi Mpya Za Usajili Barani Ulaya Leo
Liverpool yamfukuzia Lewandowski 'mpya'
Jurgen Klopp amewataka maskauti wa Liverpool kumfuatilia kinda wa Polandi wa miaka 19, Dawid Kownacki ambaye anafananishwa na Robert Lewandowski mtaifa mwenzake.
Source: The Sunday People
Tuesday, April 12, 2016 05:12
Liverpool hatarini kumpoteza Allen
Kiungo wa Wales Joe Allen anaweza kupatikana kwa uhamisho huru ifikapo 2017 kwani mazungumzo ya mkataba mpya na klabu ya Liverpool yanazidi kuzorota.
Source: BBC Sport
Tuesday, April 12, 2016 05:08
Zlatan Ibrahimovic anataka Kwenda Man United
Zlatan Ibrahimovic atakuwa tayari kutua Manchester United majira ya joto iwapo tu Louis van Gaal ataondoka Old Trafford mwisho wa msimu.
Source: Sky Sports
Tuesday, April 12, 2016 05:04
Arsenal Yamvizia Bentancur
Arsenal wamemskauti kiungo wa Boca Junior, Rodrigo Bentancur. Real Madrid nao wameonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kinda.
Source: ESPN
Tuesday, April 12, 2016 05:01
0 comments:
Post a Comment