Tuesday, April 12, 2016

Aliyoyasema Samuel Eto'o Kuhusu Leicester City Na Matumaini Ya Kuwa Mabingwa Wa EPL

Samuel Eto'o


Nyota wa zamani wa Barcelona na Inter hitman amekuwa akifuatilia ushujaa unaooneshwa na Leicester City, na anaamini meneja Claudio Ranieri ndio nyota wa mchezo

Hadithi ya Cinderella ya Ligi Kuu Uingereza “Leicester City” imempata Mpenzi mwingine. Samuel Eto'o anaonyesha wazi kuvutiwa na Kikosi hicho cha Claudio Ranieri ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kushinda taji la EPL msimu huu.

Kikosi Cha Leicester City
Licha ya matatizo yote waliyoyapata msimu wa mwaka jana Leicester City inajihakikishia kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA, shukrani pia kwa Vardy  kwa ushindi wa Jumapili 2-0 dhidi ya Sunderland wakiwa wamewaacha wapinzani wao wa karibu Tottenham kwa pointi saba.
Yamekuwa ni maajabu makubwa kutoka kuepuka kushuka daraja msimu uliopita hadi kushindania ubingwa msimu huu, shukrani kwa Claudio Ranieri. Staa huyo wa zamani wa Barcelona na Inter Millan Samuel Eto'o alionyesha kummwagia sifa Ranieri.
Claudio Ranieri

"Nilikuwa na nafasi ya kuanguka kwa upendo na mengi ya klabu hiyo, sasa mimi nipo katika upendo na Ranieri na Leicester City," alisema Eto'o, ambaye sasa yupo katika klabu ya Antalyaspor ya Nchini Uturuki.
"Jamie Vardy? Yeye ni nzuri sana, lakini pia Kocha Ranieri anaonyesha maajabu makubwa sana”

"Imekuwa ni mshangao kwa kila mtu kwa wao hakika kushindania Ubingwa wa Ligi Kuu."

Leicester, ambao walishinda mechi zao tano zilizopita bila kufungwa bao mechi dhidi ya West Ham, Swansea City, Manchester United, Everton na Chelsea wanatarajia kushuka dimbani tena kucheza na West Ham United siku ya Jumapili ya tarehe 17.

Related Posts:

  • Rasmi: Torino Yamnasa Joe Hart Mlinda Mlango namba moja wa Uingereza Joe Hart amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa mkopo akitokea Manchester City. Hart alijikuta akiwa chaguo la pili la kocha Pep … Read More
  • NYOTA WA ZAMANI WA MAN UNITED AITABIRA UBINGWA CHELSEA Paul Scholes anasema Chelsea wana nafasi ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu Nchini Uingereza. Chelsea inaongoza ligi hiyo kufuatia ushindi mnono katika mechi zake tatu ambazo imekwishacheza hadi hivi sasa chini ya kocha Mpya… Read More
  • Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kumsajili beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi. Licha ya thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutowekwa wazi lakini habari za chini chini z… Read More
  • Rasmi: Wilfred Bony Atua Stoke City Klabu ya Stoke City imekamilisha uhamisho wa Wilfred Bony kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester City. Bony aliyefeli kumshawishi kocha mpya wa City, Mhispania Pep Guardiola amefanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo 4… Read More
  • WEST BROM YAVUNJA REKODI YA KLABU USAJILI WA CHADLI Klabu ya West Bromwich Albion imevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumsajili Winga wa Tottenham Spurs kwa kitita cha Pauni milioni 13. Chadli alijiunga na Spurs akitokea FC Twente kwa uhamisho wa pauni milioni 7 Julai 2013… Read More

0 comments:

Post a Comment