Wednesday, March 1, 2017

Ruvu Shooting 0 - 2 Yanga SC , goli la Emanuel Marthin laacha gumzo Taifa


Yanga waiadhibu Ruvu Shooting 2 - 1 uwanja wa Taifa.

kikosi cha yanga kikitoka kujeruhiwa na mnyama Simba leo katika dimba la uwanja wa Taifa jiji Dar es salaam wamekata ngebe za msemaji machachari wa Ruvu Masao Bwire.

Msemaji huyo alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari jana akitoa maneno makali na yenye msisimko pale aliposema "Yanga alishauliwa lakini hajazikwa hivyo kesho lazima tuzike".

ikiwa imefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake cha leo kwa kuwaanzisha Hassan Ramadhani Kessy,  Nadir Haroub Canavaro,  Vincent Bossou, . Deus Kaseke, Geoffrey Mwashuiya, iliwachukua dakika 30 ndipo walipopata penati baada ya mlinzi wa Ruvu kuunawa mpira uliopigwa na Obrey Chirwa.

mwamuzi aliamuru ipigwe penati na Saimon Msuva aliipa Yanga uongozi wa goli moja na goli lake la 12 msimu huu.

dakika ya 45 Obrey Chirwa alifunga goli safi kwa kichwa lakini Mwamuzi alilikataa goli hilo na kumpa kadi ya njano kabla ya 46' kumtoa  nje kwa kosa la kumdharau mwamuzi.
Mpaka mapumziko mwenyeji Ruvu Shooting 0 - Yanga SC 1.

Kipindi cha pili Ruvu walikuja kwa nguvu na kukosa nafasi nyingi za wazi, 
dakika ya 93 Emanuel Marthin alifunga goli saafi kwa kichwa baada ya krosi safi kutoka upande wa kulia iliyochongwa na Msuva.

mpaka mwisho wa mchezo Ruvu Shooting 0 - Yanga SC 2.

kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha alama 52 katika michezo 23 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Simba wenye 54 baada ya michezo 23.

0 comments:

Post a Comment