Sunday, February 26, 2017

Manchester United 3 - 2 Southampton, Zlatan Ibrahimovic aipa United taji la kwanza na taji lake la 32



Manchester United wamefanikiwa kutwaa kombe la EFL baada ya kuiadhibu timu ya Southampton kwa jumla ya goli 3 – 2 katika dimba la taifa la Uingereza la Wembley.

United ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli 19’ baada ya Oriol Romeu wa Southampton kumchezea rafu mbaya kiungo wa United Ander Herrera na muamuzi kuamuru lipigwe pigo huru, Faulo hiyo ilipigwa kiufundi na Zlatan Ibrahimovic na kuiandikia United goli la kwanza.

Dakika 38 Jesse Lingard aliipa United goli la pili baada ya kuukuta mpira toka upande wa kushoto uliopigwa na Marcos Rojo.

Mpaka mapumziko United 2 – 0 Southampton. Na Manchester walitawala zaidi kipindi chwa kwanza.

Kipindi cha pili Southampton walikuja kwa nguvu na kufanikiwa kuutawala mchezo kwa kiwango kikubwa na dakika ya 45 Manolo Gabbiadini aliandikia SOTON goli la kwanza.

Dakika tatu badae 48’ Manolo Gabbiadini tena aliipatia SOTON  goli la kusawazisha.
United ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 87’ pale  Ander Herrera alipomtengea Zlatan Ibrahimovic pasi safi na yeye bila ajizi akaiandika United goli la tatu na la ushindi.





0 comments:

Post a Comment