Timu ya Barcelona
imetambatia timu ya Atletico Madrid baada ya kuichapa goli 2 - 1.
Mpira ulianza kwa kasi
kila timu ikifika langoni mwa mpinzani, 4' Diego Godin alikosa goli la
wazi.
mpira uliendelea kuwa wa
kosa ni kukose mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika kila timu ilikwenda
vyumbani na kuacha ubao ukisomeka 0 - 0.
kipindi cha pili
kilianza kwa mashambulizi ya nguvu kwa kila timu na mnamo 48' Luis Suarez
alikosa goli la wazi baada ya kupenyezewa pasi na Neymar.
51' gezma alipiga shuti
kali lakini umakini wa kipa aliweza kuokoa mpira huo. 64' rafinah anaipatia
barca bao baada ya piga nikuge langoni mwa Atletico Madrid.
dakika ya 70 Atletico
walipata faulo karibu na eneo la kumi na nane na ilipigwa kiufundi na kutua
kwenye kichwa cha Diego Godin na kuipatia timu yake goli pekee kwa siku ya
leo.
75' Angel Correa
alimfanyia rafu mbaya Jeremy Mathieu na kupewa kadi ya njano.
77' Jeremy Mathieu
anatoka nje anaingia Lucas Digne baada ya kushindwa kuendelea na mchezo
huo.
mabadiliko ya
kumuingizaAndre Gomes kuchukua nafasi ya Sergi Roberto 85' yaliongeza
mashambulizi na 86' messi anaipatia Barcelona goli la pili baada ya
kumalizia kazi aliyoifanya yeye mwenyewe na kumgonga beki wa Atletico Madrid
kabla ya kuumalizia mpira huoo.
mpaka mpira unamalizika
Atletico Madrid 1 - 2 Barcelona.
kwa matokeo hayo
Atletico wanasalia na pointi zao 45 baada ya mechi 24 katika nafasi ya 4.
Barcelona wamekwea mpaka
kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya michezo 24 wamejikusanyia pointi 54
0 comments:
Post a Comment