Thursday, February 9, 2017

Ed Woodward amtia kiburi cha kusajili Jose Mourinho, Antoine Griezmann kutua majira ya joto



Ed Woodward aridhia Jose Mourinho kufanya usajili mwingine wa kutisha majira ya joto.

Alisema “tutaendelea kutengeneza kikosi imara” kauli hiyo aliitoa leo wakati bosi huyo wa United alipokuwa anaongea na wawekezaji wa kilabu hiyo baada ya robo ya pili kukamilika.

Alisema katika robo ya pili ya mwaka United imepata faida ya £37.6m.

Mchezaji ambae huenda akatua katika dimba la Old Trafford majira yajayo ya joto ni mshambuliaji wa Atletico Madrid  Antoine Griezmann mwenye thamani ya £86m


Pia Ed Woodward alimponeza mchezaji Wayne Rooney kwa kuifikia na kuivuka rekodi ya muda mrefu ya ufungaji bora wa United wa wote iliyowekwa na Sir Bobby Charlton.

0 comments:

Post a Comment