Matuta yameamua mchezo wa yanga vs simba ndani ya uwanja wa
amani.
Mchezo ulianza kwa kasi huku kila timu ikishambulia kwa
tahadhari kubwa na kujilinda kwa haraka.
Piga nikupige zilianza pale msuva alipokokota mpira kutoka
lango la simba na kupiga mpira uliompita kipa wa simba lakini umakini wa beki
za simba zilifanikiwa kuokoa hatari hiyo isiingie wavuni.
Dakika chache baadae Mohamed Ibrahim alipiga mkwaju mzito
ulioguswa kwa ustadi mkubwa na kipa wa yanga Deo Munish na kugonga mlingoti wa
juu ila umakini hafifu wa mshambuliaji wa simba ulisababisha apige hovyo na
kuutoa nje mpira.
Mpka dakika 90 zinamalizika yanga 0 0 simba, kwa sharia za
kombe la mapinduzi hatua ya nusu fainali mchezo ukiisha kwa sare kinachofuata
ni mikwaju ya penati.
Simba ndio wa kwanza kupiga penati kupitia kwa nohodha wao
Jonas Mkude ambae alipata, yanga alianza kipa wao DEogratius Munish lakini
penati yake iliokolewa na kipa wa simba.
Penati ya pili ya simba alipiga golipa Agyei, wakati penati
ya yanga ikipigwa na msuva na wote
walipata.
Penati ya tatu ya simba ilipigwa na Mwanjali akakosa
wakati kamusoko akapata.
Penati ya nne ya simba ilipigwa na mudhamiru akapata na
upande wa yanga alipiga haji mwinyi akakosa.
Penati ya tano ya simba ilipigwa na mkongo Bokungu na
kuiwezesha simba kupata ushindi wa goli 4 kwa 2.
Simba sasa itakutana na azam fainali siku ya ijumaa 13/1/ ,
azam wao walicheza mapema na kuifunga taifa jang’ombe goli 1 kwa 0, kwenye
mchezo wa mapema.
0 comments:
Post a Comment