Tarehe 10/1/2017 mida ya saa mbili usiku katika dimba la
uwanja wa Amani hatumwi mtu sokoni pale vinara wa kundi A simba sc
itakapokutana na mahasimu wao wa jadi Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya
kombe la Mapinduzi.
Huu utakuwa ni mchezo muhimu si tu kwamba ni nusufaili ya
mapinduzi la hasha ni zaidi ya nusu fainali kwani simba na yanga ni wapinzani
hata kwa mechi ya kirafiki, mara nyingi mchezo wa simba na yanga hautabiriki na
Kitu kizuri ni ujio wa makocha wawili wa simba na yanga ,
wawili hawa watakutana kwa mara ya kwanza katika historia ya timu zao, omog
yeye kidogo anauzoefu wa kupambana na yanga akikinoa kikosi cha azam misimu
michache iliyopita, lakini lwandamina yeye haijui simba ila ni mzoefu wa ligi
mbali mbali za Afrika.
Yanga wapo na kumbukumbu ya kipigo cha aibu walichokipata
toka kwa azam katika mchezo wake wa kukamilisha hatua ya makundi hivyo
tutegemee mchezo ambao yanga watajipanga
kuwafurahisha washabiki wao.
Simba wao wanataka matokeo chanya ili kuondoa uteja ambao
umeonekana kuanza kuota mizizi kwa kipindi hiki cha miaka miwili.
Hitimisho atakaemzidi mwenzie mbinu ndio mshindi wa mchezo
huo muhimu.
Mchezo mwingine wa mapema ni kati ya azam na jong’ombe boys
kutoka visiwani Zanzibar majira ya saa kumi jioni.
0 comments:
Post a Comment