Tuesday, October 11, 2016

VIONGOZI TOTO AFRICANS WATUMBULIWA

Uongozi wa klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umewasimamisha baadhi ya viongozi wake kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Godwin Aiko, Mwenyekiti wa klabu hiyo amesema sababu kubwa ya kuwasimamisha viongozi hao ni kutokana na utovu wa nidhamu na kutomheshimu yeye kama mwenyekiti wa klabu.

Viongozi waliosimamishwa ni Isack Mwanahapa na Saleh Akida (Wajumbe wa kamati ya Utendaji).

Pamoja na hao walosimamishwa wapo wanachama ambao wamesamehewa kufuatia sakata hilo nao ni Beatus Madenge, John Kisura na Kipalata Ngasa. Wanachama hao walihusika katika vurugu katika mechi ya Toto Africans dhidi ya Yanga iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio wanachama hao walivamia gari la Katibu wao Ernest Mpio kugombea fedha za mapato ya mechi hiyo wakitaka walipwe posho ndipo gari hiyo iondoke.

“Kuhusu suala la makamu mwenyekiti Ahmed Gao ambae pia alisimamishwa bado tunalifanyia kazi,” alisema.
Gao alisimamishwa kutokana na kosa la kujitangazia kuwa avuliwe uongozi kwa muda kwa sababu ya mechi ya Yanga na Kutangaza hadharani kuwa yeye ni mwanachama wa Yanga.

Viongozi hao wanasimamishwa ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kujiuzulu kwa kocha Rogasian Kaijage aliyeifundisha timu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu akirithi mikoba ya John Tegete.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

0 comments:

Post a Comment