Tuesday, October 11, 2016

SIMBA YAPEWA ONYO MBEYA

Timu ya soka ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya siku ya jumatano kuvaana na timu ya wananchi kutoka jijini humo Mbeya City.

Kuelekea Mchezo huo, Klabu ya Mbeya City imetoa onyo kwa Wekundu hao wa Msimbazi kuwa hawatatoka salama katika dimba hilo hivyo wajipange sawasawa kwani Mbeya City wamejipanga vizuri kuondoka na Pointi tatu katika mchezo huo.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten.
Aidha Msemaji huyo aliongeza kuwa Simba isitegemee kushinda kirahisi katika mchezo huo kama walivyoshinda katika michezo yake iliyopita kwani hata wao wamejiandaa vilivyo na wanahitaji ushindi.

"Simba wajiandae vya kutosha kwa sababu tumedhamiria kufunga magoli mengi, tunajua tabia zao wanapofungwa lazima wakae" alisema Ten.

Msemaji huyo alisema kitu cha msingi kinachohitajika ni uamuzi utakaozingatia sheria 17 za mchezo ili mashabiki wapate burudani na kufurahia ushindi halali wa timu yao.

Mbeya City inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza michezo minane na kufanikiwa kujikusanyia jumla ya alama 12 zilizowaweka katika nafasi hiyo ya 4.
Dismas pia alisema wachezaji wake waliokuwa majeruhi wako fiti na wameanza mazoezi tayari kwa kuikabili Simba, wachezaji hao ni Sankhani Mkandawile na Haruna Shamte.

"Shamte na Mkandawile wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi jana, hii ni tafsiri kuwa kikosi chetu kimetimia, Simba ni timu ambayo tunaijua, hatuna shaka nao, mara kadhaa wamekuja hapa wakapata kipigo, tunafahamu wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu lakini kuchez na City ni jambo tofauti inawalazimu kujipanga sana, waje nasisi tupo tayari" alisema Ten.

Aidha Simba nao kwa upande wao, huo utakuwa ni mchezo wa kwanza kwao kucheza nje ya Dar Es Salaam huku pia ikitarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi waliloanza nalo kwa kasi tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016-17 wakiwa hawajapoteza hata mchezo mmoja.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Related Posts:

  • SAKATA LA UCHAGUZI YANGA, WAGOMBEA WAWEKEWA VIKWAZO Wote waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Yanga kupitia TFF wametakiwa kuchua fomu upya katika makao makuu ya klabu ya Yanga. Wagombea wote waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Yan… Read More
  • TFF YATANGAZA TAREHE YA KUFUNGULIWA DIRISHA LA USAJILI Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limetangaza tarehe ya kuanza kwa zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Vodacom Tanzania kuwa ni Juni 15 hadi Agosti 6, 2016. Kwa mujibu wa kalenda ya shiriki… Read More
  • YALIYOJIRI KESI YA MWINYI KAZIMOTO Kesi ya mchezaji wa Simba Mwinyi kazimoto kumshambulia na kumdhuru mwandishi wa habari imetolewa maamuzi yalimwacha huru mchezaji huyo . Kesi hiyo iliyokuwa  inayomkabili mchezaji huyo wa Simba na Timu ya Taifa, Taif… Read More
  • BEKI WA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI KUTUA SIMBA Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Hans Poppe yupo katika mazungumzo na Beki wa kati wa klabu ya Black leopards ya nchini Afrika kusini Harry Nyirenda. Hans Pope yupo nchini Zimbabwe kukamilisha usajili wa kocha Kalist… Read More
  • WASANII, WANAMICHEZO WATENGEWA BILIONI 3 Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 3 kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya michezo, sanaa na ubunifu. Pesa hizo zimetengwa na serikali katika mwaka ujao wa fedha,kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa fedha na uchum… Read More

0 comments:

Post a Comment