Saturday, August 6, 2016

RASMI: MANCHESTER CITY YAMNASA MORENO

Klabu ya Manchester City iliyo chini ya kocha Mpya Pep Guardiola imekamilisha uhamisho wa kinda Mkolombia Marlos Moreno.

Moreno 19, ametua katika dimba la Etihad akitokea Atletico Nocional na amesaini mkataba wa miaka mitano.

Hata hivyo Moreno atapelekwa kwa mkopo katika klabu ya Deportivo La Coruna ya nchini Hispania na ataitumikia klabu hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2016/17.
Baada ya usajili huo kukamilika Moreno aliyasema haya;

"Pep Guardiola ni moja ya makocha bora zaidi duniani. Nafikiri anapenda sana wachezaji makinda na anauwezo wa kukuza vipaji vyao. Ni faraja kwangu kufanya kazi na Pep na kuwa sehemu ya timu kubwa"

Moreno anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa katika klabu hiyo, wengine wakiwa ni Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito, Oleksandr Zinchenko, Gabriel Jesus and Aaron Mooy.

Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

0 comments:

Post a Comment