Sunday, August 14, 2016

KAULI ZA MAKOCHA YANGA,MO BEJAIA BAADA YA MECHI JANA

Mchezo kati ya Yanga na MO Bejaia jana umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli moja kwa sufuri.
Matokeo hayo yamefufua matumaini ya Yanga kuwania kucheza hatua ya Nusu fainali kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC), hata hivyo matumaini hayo yanategema matokeo ya mchezo wa leo kati ya Medeama dhidi ya MO Bejaia, na dua za Wanayanga wengi leo ni kuiombea ushindi klabu ya TP Mazembe huku wao wakitakiwa kuifunga TP Mazembe katika mchezo wao wa Mwisho wakati huo pia mchezo kati ya MO Bejaia na Medeama watoe Sare.

Baada ya kumalizika mchezo wa Jana, makocha wa timu zote Mbili waliyasema yafuatayo;

"Mwanzo tulikuwa tunauoga Kidogo, lakini kipindi cha pili tulitulia na kutengeneza nafasi nyingi, Kwa Bahati Mbaya hatukuweza kuzitumia nafasi hizo, Sasa hivi tunasubiri matokeo ya mechi kati ya Medeama-Mazembe tuone kama bado tutakuwa na nafasi ya kufuzu, lakini vyovyote itakavyokuwa tutapambana na kushinda mechi ya mwisho" Alisema Kocha Wa Yanga, Hans Van Pluijm Baada ya Kumalizika kwa mchezo wa jana.

"Tuliuchukulia mchezo kwa Umakini Mkubwa sana, Kwa Bahati mbaya hatujashinda. Mipango yetu imevurugwa kwa sasa na tunatakiwa kupambana kwa nguvu zetu zote kushinda katika mchezo wetu wa Mwisho" alisema Nasser Sandjak Kocha Mkuu wa timu ya MO Bejaia jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Jana.
Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA 

0 comments:

Post a Comment