Friday, August 5, 2016

JAMES MILNER AACHANA NA TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA

James Milner amestaafu kuitumikia timu yake ya taifa baada ya mazungumzo aliyofanya na Kocha mpya wa timu hiyo Sam Allardyce.

Milner 30, anaachana na kikosi cha England akiwa ni mmoja kati ya wachezaji walioiwakilisha nchi hiyo katika michuano minne mikubwa ikiwemo Euro 2016 iliyomalizika hivi karibuni huko nchini Ufaransa.

Kiungo huyo wa Liverpool ametoa nafasi kwa kizazi kipya kutoa mchango wao katika kikosi hicho cha England na tayari Shirikisho la mpira wa miguu nchini humo limetangaza uamuzi huo wa Milner leo Ijumaa Agosti 5,2016.

"Napenda kutoa shukrani zangu kwa Sam kwa kukutana na mimi na kulizungumzia suala langu na hatimaye kufikia makubaliano" alisema Milner.

"Nadhani maamuzi tuliyoyafikia ni kwa lengo zuri tu kwa taifa. Namtakia Sam, Wachezaji, Viongozi wote pamoja na mashabiki mafanikio mema hapo mbeleni" aliongeza Mkongwe huyo anayekipiga katika klabu ya Liverpool.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA 

0 comments:

Post a Comment