Thursday, June 2, 2016

YANGA YAPINGA TFF KUINGILIA UCHAGUZI WAO

Klabu ya Yanga imepinga suala la TFF kuonekana kuingilia uchaguzi wao na kusema wao watafanya uchaguzi wao wenyewe.




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF lilitangaza kuwa mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Yanga unasimamiwa na Shirikisho hilo kwa mujibu wa utaratibu waliokautoa hapo awali, lakini klabu ya Yanga imeibuka na kusema wanapingana na kauli hiyo ya TFF na kwamba uchaguzi utasimamiwa na wao wenyewe na kamwe hawatoweza kukubali uchaguzi huo usimamiwe na TFF ambayo inajumuisha watu mbalimbali wengine wakiwa sio wanayanga.

TFF ilitoa tarehe ya uchaguzi wa Yanga kuwa ni Juni 6 lakini Yanga nao wametoa ratiba ya matukio yote ya uchaguzi huo na katika kalenda yao inaonyesha uchaguzi utafanyika Juni 11 badala ya 6 ambayo ilitangazwa na TFF.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Baraka Deudiet amesema kamati ya uchaguzi na bodi ya wadhamini imemwagiza kutangaza tarehe yao ambayo watafanya uchaguzi na sio ile ya TFF

"Nimepewa maelekezo na kamati ya uchaguzi ya Yanga na bodi ya Wadhamini kutangaza mchakato wa uchaguzi wa klabu yetu kama tulivyotakiwa na serikali kufanya hivyo baada ya kuwaandikia TFF lakini tunashangazwa na TFF hao kutangaza mchakato wa uchaguzi wetu kinyume na inavyotakiwa" alisema Baraka.


0 comments:

Post a Comment