Thursday, June 2, 2016

YUSUF MANJI , CLEMENT SANGA KUTETEA NAFASI ZAO YANGA

Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji Pamoja na Makamu Mwenyekiti Bw. Clement Sanga wanatarajiwa kukuchukua fomu leo kutetea nafasi zao za uongozi katika klabu hiyo.




Bw. Yusuf Manji na Clement Sanga pamoja na wanachama wengine wa Yanga watachukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Yanga kufuatia uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.
Zoezi hilo la uchukuaji wa Fomu litafanyika leo saa sita mchana katika makao makuu ya Klabu ya Yanga.

Manji na Sanga ambao ndio viongozi wa juu kwa sasa katika klabu hiyo wanarudi tena kutetea nafasi zao baada ya muda wao wa uongozi kuelekea ukingoni.
Kwa mujibu wa kalenda na matukio ya uchaguzi wa Yanga zoezi la uchaguzi litafanyika Juni 11 na matokeo kutangazwa Juni 12, 2016.

0 comments:

Post a Comment