Friday, June 10, 2016

YANGA KUANZA KAMBI RASMI LEO

Timu ya Dar Young Africans inatarajiwa kuingia kambini leo kujiandaa na michezo ya hatua ya makundi CAF Confederation Cup.


Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza katika hatua hiyo Juni 19 dhidi ya MO Bejaia ya nchini Algeria, mchezo utakaopigwa huko Algeria majira ya saa 4 usiku kwa Algeria sawa na Saa 6 usiku saa za Afrika Mashariki.

Akizungumzia maandalizi hayo Meneja wa Yanga Hafidi Salehe amesema, wataweka kambi Dar Es Salaam na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya maadalizi hayo.

"Kesho (leo) tunatarajia kuingia kambini Dar Es Salaam kwa ajli ya maandilizi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika, kujiimarisha na kuhakikisha tunajiweka sawa kwa mazoezi tayari kwa mchezo wetu wa kwanza tutakaocheza" alisema Meneja huyo.

Wachezaji wote wa Yanga wapo kikosini hapo isipokuwa Vicent Bossou ambaye anatarajiwa kuwasili wakati wowote akitokea kwao Togo. Salehe alisema kiujumla maandalizi yao yanakwenda vizuri na kwamba uchaguzi unaoendelea Yanga hauwezi kuathiri mipango yao ya kujiandaa kwenda kuwakilisha vyema katika michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment