Mchezo huo utapigwa uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaam jumapili Juni 26, 2016.
Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime amesema wataondoka na pointi tatu katika mchezo huo kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya.
"Naamini kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari ya kwenda Madagascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya." alisema Shime.
Mchezo huyo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Ethiopia ambao ni Belay Asserese (Mwamuzi wa kati), Tigle Belachew na Kinfe Yilma (Waamuzi wasaidizi), huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Lemma Nigussie na kamishna wa mchezo huo ni Bester Kalombo.
0 comments:
Post a Comment