Rais Wa Simba Evans Aveva |
Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kulivalia njuga suala hilo ili kubaina nani hasa anayeihujumu klabu yao.
Rais wa klabu hiyo, Evans Eveva amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo wakimtuhumu mmoja kati ya viongozi wa Simba kwamba anaihujumu timu yao na kwamba suala wao kama uongozi hawatalipuuzia.
"Leo Kamati ya utendaji ya Simba itakutana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo maadalizi ya mkutano mkuu wetu mwezi ujao, lakini pia kuna tuhuma kwa kiongozi mwenzetu zinatoka kwa wanachama hili nalo tutalijadili." alisema Aveva.
Aidha Rais huyo amesema baada ya kikao hicho wataweka wazi mambo yanayohusu mkutano wa wanachama wa klabu hiyo.
"Baada ya hapo kila kitu tutaweka wazi masuala ya kadi zitakazotumika, taratibu zote za mkutano tutaweka wazi: alisema kiongozi huyo.
Kumekuwa na mikutano mbalimbali ya wanachama wa Simba katika matawi mbalimbali, mikutano ambayo Aveva amekuwa akihudhuria na kwamba kilio kikubwa cha wanachama hao ni kwamba kuna kiongozi anaihujumu klabu yao.
Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa
0 comments:
Post a Comment