Wednesday, June 1, 2016

PAUL NONGA ANYOOSHA MIKONO YANGA

Mchezaji aliyejiunga na Yanga akitokea Stand United Paul Nonga amesema ameuomba uongozi wa Yanga umuuze.




Nonga amefikia uamuzi huo baada ya kukosa nafasi ya kucheza muda mwingi katika klabu hiyo.

”Nimeomba kuuzwa na tayari barua ipo mezani kwenye ofisi ya Yanga na nimewatajia mahali ninapopenda kuuzwa, nimeomba kuuzwa ili wasiingie hasara kwasababu walininunua kwa pesa nyingi. Sababu kubwa ya maamuzi Yangu haya ni nafasi finyu ya kucheza niliyonayo katika kikosi cha Yanga kutokana na ubora walionao wenzangu wanaocheza nafasi niichezayo na wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki nafasi hiyo”, amesema Nonga.

Aidha Nonga amesema uamuzi huo umetokana na utashi wake yeye mwenyewe hakuna mtu yeyote aliyemlazimisha na amefanya hivyo maslahi yake na ya Yanga pia.

0 comments:

Post a Comment