Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma ameanza kuwindwana vigogo wa soka la Misri na Afria timu ya Al Ahly.
Ngoma amekuwa mshambuliaji tishio sana katika klabu ya Yanga na ametoa mchango mkubwa sana katika mafanikio waliyoyapata Yanga msimu huu. Amefunga jumla ya mabao 17 katika msimu wa ligi kuu Vodacom 2015/16, huku pia akiwafunga Al Ahly katika mchezo wa klabu bingwa Afrika uliochezwa Misri.
Al Ahly wameonyesha kuvutiwa na nyota huyo na kwamba wapo tayari kuingia sokoni kuiwinda saini yake mwishoni mwa msimu huu.Mapharao hao wanafikia hatua hiyo ya kumuhitaji Ngoma kufuatia wachezaji wao John Antwi wa Ghana na Malick Evouna wa nchini Gabon kushindwa kuonyesha kiwango bora.
Donald Ngoma mwenyewe ameonyesha utayari wake endapo Al Ahly watatuma ofa ya kumuhitaji katika klabu yao.
"Kwanini Hapana?, Ni klabu kubwa katika Afrika na nitakuwa tayari kwenda Misri" alisema Ngoma alipohojiwa na Marwan Ahmed wa Kingfut.com.
Yanga watakuwa na kibarua kizito cha kusaka mbadala wa Ngoma endapo wataamua kumuuza kwa Mapharao kwani amekuwa ni kivutio na mchango mkubwa katika klabu yao.
0 comments:
Post a Comment