Kipre Tchetche mchezaji wa Azam FC raia wa Ivory Coast amesema inatosha sasa kucheza Tanzania hivyo anataka kwenda kujaribu sehemu nyingine.
Kipre ambaye ana mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake ametosheka na muda aliokaa nchini akicheza ligi kuu Vodacom. Kipre ameyasema hayo akiwa kwao nchini Ivory Coast alikokwenda kwa mapumziko.
"Inatosha kwa muda ambao nimecheza Tanzania, nahitaji kuondoka kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine. Nimekuwa na maisha mazuri sana Azam, viongozi na wamiliki wanajali sana wachezaji, lakini nalazimika kuyaacha yote" alisema Tchetche alipozungumza na Bin Zubeiry.
Kipre Tchetche yupo nchini Ivory Coast kwa mapumziko na tetesi zinasema nyota huyo ameshasaini mkataba na klabu moja ya Uarabuni.
0 comments:
Post a Comment