Wednesday, June 1, 2016

MUNAODHANI KIPRE TCHETCHE ATAJIUNGA NA YANGA, HII NDO KAULI YAKE KWENU

Mchezaji Kipre Herman Tchetche amesema hana mpango wa kujiunga na klabu nyingine yoyote ya Tanzania.




Tchetche amefikia hatua ya kuyazungumza hayo kufuatia uvumi unaotawala hivi sasa ukimuhusisha yeye kujiunga na klabu ya Yanga mara baada ya kutoka Azam FC. Tchetche amesema imetosha kucheza Tanzania na hivi sasa anaangalia changamoto mpya sehemu nyingine, Huku akisisitiza kwamba habari zinazoenea kwamba atajiunga na Yanga ni za Uzushi na ni za kuzipuuza.

"Nitoke Azam, niende Yanga?, Usinifanye nicheke, mimi nimesema sitaki kuendelea kucheza Tanzania na hadi sasa sijasaini kokote hadi nipewe ruhusa na uongozi wa Azam" alisema Kipre Tchetche akiwa kwao nchini Ivory Coast.

Kipre amekuwa mchezaji muhimu sana katika kikosi cha Azam FC na uwezo wake wa kufunga magoli ndio unawafanya mashabiki wa soka hasa wa Yanga kumhusisha na kujiunga na klabu hiyo ambayo inahitaji kuimarisha kikosi chake ili kiweze kuwakabili vizuri wapinzani wao katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambayo kwa sasa imefikia hatua ya makundi.

Licha ya Tchetche Mwenyewe kudai hataki tena kucheza soka la Tanzania kwa upande wao Azam FC wamesema Kipre ni mchezaji halali wa Azam FC na wanashangazwa na uzushi kwamba Tchetche anatimkia  Yanga.

"Sijui nani anazusha haya mambo, Kipre ni mchezaji wa Azam FC, hakuna timu inayoweza kumsajili pembeni zaidi ya kufuata utaratibu, Kwa ufupi Kipre ni mchezaji halali wa Azam FC, full stop" alisema Jaffar Idd msemaji wa Azam FC

0 comments:

Post a Comment