Wiki chache zilizopita soka24 iliripoti juu ya kifo cha Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Sajini kinyogori, Taarifa za uchunguzi zimebaini kuwa mkewe amehusika na mauaji hayo.
Sajini Kinyogori aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwao eneo la Mwadenge, Mkoani Pwani, Wauaji wa Askari huyo hawakuweza kubainika mara moja, lakin ripoti za hivi karibuni kutoka kwa kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar Es Salaam Simon Siro zinasema kwamba, Mke wa Askari huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi, amekiri kuhusika na mauaji hayo ya mumewe.
Kamanda Siro amesema Mwanamke huyo yupo chini ya ulinzi wa Askari Polisi pamoja na watuhumiwa wengine wakichukuliwa maelezo.
0 comments:
Post a Comment