Tuesday, May 24, 2016

YAJUE WALIYOYASEMA MAKOCHA WA TIMU ZINGINE KUHUSU YANGA BAADA YA MATOKEO YA DRAW YA LEO

Draw ya kuzipata timu zitakazowakilisha makundi katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika imefanyika leo Mei 24, 2016 katika makao makuu ya CAF Cairo nchini Misri.

Patrice Carteron Kocha Mkuu TP Mazembe

Katibu Mkuu Wa CAF Hicham El Amran aliongoza draw hiyo huku akisaidiwa na Madg Shams El Din, Rais wa kamati ya Marefarii (waamuzi) pamoja na Mohamed Raouaroua, Makamu wa Rais kamati ya CAF.

Soka24 ilinasa kauli zote za Viongozi mbalimbali wa vilabu vitakavyowania kutinga hatua ya nusu fainali na hapa chini nimekuwekea yote waliyoyasema baada ya draw hiyo;

Group A

Frederic Kitengie (Meneja Wa Timu Ya TP Mazembe)
"Draw ni nzuri. TP Mazembe tutacheza mechi yetu ya kwanza Lubumbashi dhidi ya Medeama ya nchini Ghana, halafu Young Africans ya Tanzania. Ni matumaini yetu kuwa tutafuzu hatua hii na kutinga nusu fainali na hatimaye kushinda kabisa kombe hili ili kuwapa furaha mashabiki wetu"

James Essilfie (Mkurugenzi Mkuu, Medeama)
"Tumefurahia hii draw. Timu zingine katika kundi letu zitaifanya timu yetu kuonyesha kiwango bora zaidi. Nyingi ya timu hizo ni zile ambazo zilitilia mashaka uwezo wetu hasa pale tulipokatoka sare dhidi ya Sundowns katika mechi yetu ya kwanza katika mzunguko wa 8, lakini tulionyesha ubora wetu. Hii draw itatuhamasisha sana na ninahakika tutafika mbali. TP Mazembe kwa sasa haiko vizuri kama ilivyokawa hapo nyuma. Ni kawaida yetu kuonyesha kiwango kikubwa kila tunapocheza na timu kubwa. MO Bejaia iliwaondosha mabingwa wa Ghana Ashantigold na tunaamini tutalipa kisasi cha ndugu zetu. Young Africans inafundishwa na Hans Van der Pluijm, Kocha wa zamani wa Medeama na kucheza dhidi yao litakuwa jambo la kufurahisha sana."

Group B

Sofiane El Bouatlaoui (Meneja wa timu ya Kawkab) 
"Tumefurahishwa sana na hii draw. Tunaamini kabisa kuwa tutafika nusu fainali. Ni kundi lenye timu nyingi za kaskazini na wote tutakumbana na changamoto ya mfungo wa mwezi wa Ramadhan"

Hussen Em Tlesh (Meneja wa Timu ya Ahly Tripoli)
"Sina mengi ya kusema kuhusu hii draw. Tumefurahishwa na jinsi ilivyoendeshwa kwa sababu wote ni wa kaskazini. Ni matumaini yetu kuwa michezo hii itasaidia kuwaunganisha Walibya"

0 comments:

Post a Comment