klabu ya Liverpool na Manchester United zimepigwa faini na UEFA kutokana na vurugu za mashabiki wao walizozifanya katika mchezo wa Europa league hatua ya 16 bora.
Klabu Zote zimekumbana na faini hiyo baada ya mashabiki wao kurushiana vitu uwanjani hapo jambo lililoonekana kuwasumbua watu wengine waliokwenda uwanjani hapo kwa lengo la kutazama mechi hiyo.
Liverpool imepigwa faini ya paundi elf 43,577 na United imepigwa faini ya paundi elf 44,342.
Liverpool pia inatakiwa kulipa hasara zote zilizosababishwa na mashabiki wake hapo Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment