Monday, May 9, 2016

TAZAMA MASHABIKI WA SIMBA WALIVYOLIANZISHA MSIMBAZI


Kufuatia matokeo mabaya yanayoikumba klabu ya Simba katika mechi zao za hivi karibuni, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wameshindwa kuvumilia na kuamua kujikusanya katika makao makuu ya klabu hiyo kwa kile wanachodai kuwa ni kutaka kujua nini mustakabali wa timu yao.
Achana na tukio la kioo cha gari lao Youtong kupasuliwa, toka asubuhi ya leo wanachama na mashabiki wa Simba SC walijazana makao makuu ya klabu yao wakihitaji ufafanuzi wa mambo wanayoyaona hayako sawa ikiwemo pia taarifa ya FIFA kuiamuru klabu hiyo kumlipa Musoti ndani ya siku 30 vinginevyo klabu hiyo itashushwa daraja.

TAZAMA HAPA HALI ILIVYOKUWA MITAA YA MSIMBAZI LEO

0 comments:

Post a Comment