Wednesday, May 18, 2016

SERENGETI BOYS YAGAWA DOZI INDIA



Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 17, 2016 imechanua vema baada ya kuilaza India mabao 3-1 katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani katika dakika ya 21 wakati lile la pili India walijifunga baada ya beki wake kuhangaika kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28 wakati lile la tatu lilifungwa na Asad Juma katika dakika ya 48 huku lile la India likifungwa na Komal Thatal katika dakika ya 38.

Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa wanasubiri angalau sare au ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini utakaopigwa Alhamisi Mei 19, 2016 na Malaysia Mei 21, 2016 ili icheze nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Mei 12 kabla ya kufikia fainali zake Mei 26, mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoka sare ya Marekani ya bao 1-1.  

Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliwakilishwa na Ramadhani Kabwili, Ally Nganzi, Ally Msengi, Asad Juma, Dickson Job, Issa Makamba, Maziku Amani, Nickson Kibabage, Shaaban Ada, Syprian Mtesigwa na Mohammed Abdallah.

India: Mohammed  Nawaz, Reamsochung Aimol, Boris Singh, Mohammed Khan, Juendra Singh, Suresh Wangjam, Amarjit Kiyam, Khumanthem Meetei, Sandjev Staldi, Aniket Jadhav na Komal Thatal.

Matokeo haya yanapatikana pia kupitia link za:

Indian Football Team Official FB page: https://www.facebook.com/TheIndianFootballTeam/

Related Posts:

  • YALIYOJIRI KESI YA MWINYI KAZIMOTO Kesi ya mchezaji wa Simba Mwinyi kazimoto kumshambulia na kumdhuru mwandishi wa habari imetolewa maamuzi yalimwacha huru mchezaji huyo . Kesi hiyo iliyokuwa  inayomkabili mchezaji huyo wa Simba na Timu ya Taifa, Taif… Read More
  • SAKATA LA UCHAGUZI YANGA, WAGOMBEA WAWEKEWA VIKWAZO Wote waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Yanga kupitia TFF wametakiwa kuchua fomu upya katika makao makuu ya klabu ya Yanga. Wagombea wote waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Yan… Read More
  • WASANII, WANAMICHEZO WATENGEWA BILIONI 3 Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 3 kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya michezo, sanaa na ubunifu. Pesa hizo zimetengwa na serikali katika mwaka ujao wa fedha,kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa fedha na uchum… Read More
  • AARON NYANDA AJIENGUA UCHAGUZI YANGA Nyanda aliyekuwa anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, amejitoa kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika kesho Juni 11, 2016. Nyanda ambaye alichukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye ofisi za shirikisho la mpira w… Read More
  • PLUIJM AWACHIMBA MKWARA WACHEZAJI YANGA Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko baada ya fainali ya kombe la shirikisho TFF, Kocha Pluijm ametoa onyo kwa wachezaji wote ambao watachelewa kufika kikosi hapo. Yanga wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa kwa… Read More

0 comments:

Post a Comment