Mashabiki wa timu ya Eskihirspor ya nchini Uturuki wamechoma moto uwanja wao wenyewe kufuatia kipigo cha goli 2 – 1 kilichopelekea timu hiyo kushuka daraja.
Imeelezwa pia katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa, timu hiyo ilikuwa ipo katika hatari ya kushuka daraja lakini baada ya kipigo hicho ndo ikawa rasmi kwa timu hiyo kushuka licha ya kuwa wamebakiza mchezo mmoja katika ligi hiyo.
Ripoti zaidi zinasema kuwa mashabiki wa timu hiyo walishakataa timu yao kucheza katika uwanja huo na kuitaka timu hiyo kuhamia katika uwanja mpya ambao tayari ulishakuwa umekamilika.
0 comments:
Post a Comment