Wednesday, May 25, 2016

LOUIS VAN GAAL APATA KIBARUA KIPYA

Kocha aliyetimuliwa hivi karibuni katika klabu ya Manchester United Louis Van Gaal amepewa Ofa nyingine mara tu baada ya kufukuzwa klabuni hapo.


Louis Van Gaal wakati anapewa kibarua katika klabu ya Man United alisema hiyo ndo itakuwa timu yake ya mwisho atakayokaa kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa kabla hajastaafu,  lakini hayo hayajatimia baada ya kufukuzwa hata kabla ya mkataba wake kumalizika.

Van Gaal alimuahidi mkewe kuwa  baada ya mkataba wake wa miaka mitatu kumalizika United atastaafu kazi ya ukocha na wataenda kuishi katika nyumba yao iliyopo nchini Ureno maisha ya raha na familia yake. Ndoto za Van Gaal hazijatimia na kufanya lengo lake la kustaafu baada ya kutoka United kuendelea kusubiri maamuzi mengine.

Imekuwa bahati mbaya kwa Louis Van Gaal baada ya kutangazwa kufungishwa virago licha ya kuwapa ubingwa wa FA Cup na tayari  ameshasafiri na familia yake ambapo kwa sasa wapo katika nyumba yao iliyoko huko nchini Ureno kwa mapumziko.

Haujapita muda mrefu tangu afukuzwe ni takribani siku 2 tu na tayari timu ya taifa ya Uholanzi imeshampa ofa Van Gaal ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika kikosi hicho kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la nchini humo. Chama cha mpira wa miguu nchini humo KNVB kinatambua umuhimu na mchango wa Van Gaal katika timu ya Uholanzi na kimeamua kumpa ofa ya kujiunga tena na timu hiyo. Van Gaal alifanya vizuri sana alipokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Brazili mwaka 2014.

0 comments:

Post a Comment