Mlinda Mlango wa Yanga Ally Mustapha amemaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Dar Young Africans na amesema yupo tayari kuongeza mkataba klabuni hapo endapo maslahi yake yataboreshwa.
Barthez katika misimu minne aliyoitumikia Yanga ameonyesha uwezo mkubwa licha ya mapungufu madogo madogo huku akifanikiwa kushinda Mataji mawili ya ligi kuu, Moja la Shirikisho pamoja na ngao ya hisani.
Ally Mustapha amesema yupo tayari kukaa mezani na Yanga ili kufikia muafaka wa hatima yake klabuni hapo huku akionyesha nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.
"Nimekuwa na mafanikio makubwa hapa Yanga kwa misimu 4 niliyocheza, ambapo ndani yake nimejenga uaminifu kwa makocha wote waliopita na huyu wa sasa lakini pia nimekuwa na marafiki wengi wachezaji na viongozi hivyo sioni sababu ya kuondoka" alisema Barthez alipozungumza na Goal.
Yanga imefanikiwa kutinga katika hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika wakiwa wamepangwa kundi moja na TP Mazembe, MO Bejaia na Medeama, hivyo wanalazimika kukisuka vizuri kikosi chao ili kuleta ushindani katika hatua hii na hatimaye kutinga hatua inayofuata ya nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment