Kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) zinaeleza kuwa timu ambazo zitatolewa katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitashuka katika Kombe la Shirikisho ambapo huko zitakutana na timu nane zilizosonga mbele ambapo zitacheza mechi za mtoano za nyumbani na ugenini kisha zitakazofuzu zitaingia hatua ya makundi.
Baada ya Yanga kutolewa, sasa itakutana na Sagrada Esperança baada ya droo kupangwa jana huku Yanga ikitakiwa kuanzia nyumbani wiki ya Mei 6-8, mwaka huu na marudio ni Mei 17-18, 2016.
0 comments:
Post a Comment