Friday, April 22, 2016

Serengeti Boys Kucheza Na Timu Ya Taifa Ya Marekani U17


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini India (AIFF) limetoa ratiba ya michuano ya vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) itakayoanza kutimua vumbi Mei 15 -25 katika mji wa Goa nchini India kwa Serengeti Boys kufungua dimba na Marekani.

Michuano ya AIFF inashirikisha timu tano za vijana wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi za Korea Kusini, Marekani, Malysia, Tanzania na wenyeji India.

Mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa kuanzia Mei 15, ambapo Tanzania itacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Marekani, huku mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji India dhidi ya Malysia.

Serengeti Boys watashuka dimbani tena Mei 17, kucheza na wenyeji India mchezo wa kwanza, Mei 19 Serengeti Boys watacheza dhidi ya Korea Kusini na mchezo wa mwisho watamaliza dhidi ya Malysia Mei 21.

Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25 ambapo kabla ya mchezo wa fainali, utchezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa.

Kikosi cha Serengeti Boys kianatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 kujiandaa na michuano hiyo ya vijana na kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani nchini Madagascar.

Related Posts:

  • Yanga Na Mwadui, Azam FC Na Mtibwa Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League ( VPL ) inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa mechi mbili. Yanga iliyotoka kumenyana na Al Ahly juzi itawakaribisha vijana wa Jamhuri Kiwelu Julio … Read More
  • Kiiza, Juuko Murshid Kikaangoni Msimbazi Tayari Simba wameanza kuangushiana lawama za chinichini. Jambo ambalo si sahihi lakini wapo ambao walikuwa chanzo cha kuua umoja katika mechi hiyo au kutokuwa makini, kukachangia wao kung’oka. Kiiza&Juuko kikaangoni:… Read More
  • Afya Ya Kapombe Yazidi Kuimarika BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, anaendelea vema na matibabu nchini Afrika Kusini huku ikielezwa kuwa afya yake inazidi kuimarika kadiri siku zinavyosogea. Kapombe yupo jiji… Read More
  • Yanga Na Azam Fc Zasusia Ratiba Kombe La FA Hili ndo Kombe La ASFC Yanga na Azam Fc zimesusia Ratiba ya michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya nusu fainali iliyopangwa kufanyika  April 24 mwaka huu. Timu zote zimetoa sababu ya kushiriki michuano ya kum… Read More
  • Kombe La FA Ngoma nzito.... Angalia matokeo ya droo hapa.Droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali, leo imepangwa. Mwadui FC imepangiwa Azam FC na mechi ya kwanza itachezwa mjini Shinyanga wakati Yanga wao watacheza na Coastal Union ambao wataanzia mjini Tanga. … Read More

0 comments:

Post a Comment