Friday, April 22, 2016
Hizi Ndio Takwimu Za Sagrada Esperanca Watakaocheza Na Yanga
Jina Kamili: Grupo Desportivo Sagrada Esperança
Kuanzishwa: 22 December 1976; miaka 39 sasa
Sagrada Esperança ni klabu inayocheza ligi kuu ya nchini Angola, maarufu kama Girabola. Kiufupi ni kwamba, timu hii imewahi kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu ya Angola mara moja (mwaka 2005) tangu ianzishwe, na mwaka 2008 ilishuka daraja. Ilipanda tena mwaka 2009.
Ligi Kuu ya mwaka jana ilishika nafasi ya kumi (10) na ilipata uwakilishi wa CAF kupitia kombe la shirikisho la nchi hiyo. Ni kama huku kwetu Coastal Union abebe Kombe la Shirikisho, basi mwakani atacheza CAF Confederation Cup, licha ya kwamba inashika mkia wa Ligi.
Ligi Kuu ya msimu huu inashika nafasi ya 10 kama unavyoona kwenye msimamo. Mbali na ubingwa huo wa mwaka 2005, timu hii imeshika nafasi za 4 2007 na nafasi ya 5 mwaka 2013. Miaka mingine yote imekuwa ikishika nafasi ya 6 kushuka chini.
Ni timu inayotumia jezi za kijani, na logo ya klabu yao ni kijani na nyota ya njano.
0 comments:
Post a Comment