Winga chipukizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, leo Ijumaa ameondoka nchini Tunisia kuelekea Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humu na atarejea jijini Dara es Salaam May 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha.
KILA LA KHERI FARID
0 comments:
Post a Comment