Hatimaye kocha wa Leicester city Claudio Ranieri amewaambia wachezaji wake kupigania ubingwa wa ligi kuu msimu huu, yeye pia akiamini timu yake ndo itaibuka mabingwa wa ligi hiyo.
Mtaliano huyo anaeinoa Leicester alifanya mkutano na wachezaji wake akiwasisitiza kupambana kikamilifu ili wahakikishe wanalitunza gepu lao la pointi 5 na mwishowe kuibuka mabingwa.
Ranieri alimtania kocha wa Tottenham Mouricio Pochettino kwamba awe mpole kwani ubingwa ni wa Leicester lakini huku akiamini kuwa Tottenham wanauwezo wa kushinda mechi zote za ligi zilizobaki.
Kwa miezi kadhaa Ranieri amekuwa akikataa kutoa hatima ya Leicester hasa alipokuwa anaulizwa endapo anaamini klabu yake hiyo inaweza ikachukua taji hilo, lakini ameamua sasa kuvunja ukimya na kusema wazi kuwa anaamini timu yake itachukua ubingwa.
“Tayari tupo katika nafasi ya kushiriki mashindano ya Champions League (UEFA), inafurahisha” alisema Ranieri “Pongezi kwa watu wote walioisaidia Leicester hadi hapa ilipofikia, Wamiliki, mashabiki, wachezaji, stafu nzima ya Leicester na kila mtu alieshiriki kwa namna moja au nyingine kuifikisha timu hapa ilipo kwa sasa, ni mafanikio makubwa sana” aliongeza Ranieri.
“Na sasa hivi tunasonga mbele lengo letu likiwa ni kushinda taji la ligi kuu. Na ndio kilichobaki kwa sasa, Mauricio, kaa kimya” alitania Ranieri akimwambia kocha wa Tottenham akae kimya akimaanisha ubingwa ni wa Leicester.
Tottenham waliongeza presha kwa kocha huyo wa Leicester baada ya ushindi wao wa 4-0 walioupata jumatatu ambao ulipunguza gepu la pointi kutoka 8 hadi 5 baada ya Leicester kutoka sare na West Ham United huku Jamie Vardy akitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment