Wednesday, April 6, 2016

TAARIFA KWA WANAOSUBIRI MECHI KATI YA YANGA NA AL AHLY

Uongozi wa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans leo April 6 kupitia kwa afisa habari wake Jerry Muro ameongea na vyombo vya habari na kuelezea taarifa za mchezo wao wa klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa April  9 2016 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Jerry amethibitisha  Al Ahly kuwasili Dar Es Salaam alfajiri ya leo, pamoja na CAF kutoa majina ya waamuzi wa mchezo huo ambao wanatoka Ivory Coast Denis Dembele, Mauris Donatien, Moussa Bayere, Tangba Kambou lakini kamisaa wa mchezo Celestine Ntangungira anatokea Rwanda.


Jerry Muro

Hadi sasa Yanga mechi zao zilizopita za klabu Bingwa Afrika waligoma zisioneshwe kwenye TV ” Kwa sasa viongozi wanafanya utaratibu wa kuangalia namna ambavyo tunaweza kuruhusu TV kuonesha mchezo huo, lakini watu wajue tutaruhusu matangazo ya TV yarushwe mikoani kasoro Dar na Pwani ndio maana tumeweka kiingilio cha chini elfu tano” >>> Jerry Muro

Related Posts:

  • MARUFUKU SIMBA NA YANGA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA Serikali yatoa katazo juu ya simba na yanga kuuutumia uwanja wa taifa na kuwaambia watafute pakuchezea mechi zao. Hayo yamesemwa na waziri anaehusika na michezo mheshimiwa Nape.Nape alisema hivi “Uwanja huu sasa hautatumik… Read More
  • SIMBA YAPEWA ONYO MBEYA Timu ya soka ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya siku ya jumatano kuvaana na timu ya wananchi kutoka jijini humo Mbeya City. Kuelekea Mchezo huo, Klabu ya Mbeya City imetoa onyo kwa Wekundu h… Read More
  • MCHEZO WA STARS NA ETHIOPIA WAYEYUKA Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa soka nchini limeota mbawa baada ya shirikisho la soka la Ethiopia kuiandikia TFF kuwa mchezo huo hautakuwepo kutokana na sababu za kiusalama nchini Ethiopia… Read More
  • VIONGOZI TOTO AFRICANS WATUMBULIWA Uongozi wa klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umewasimamisha baadhi ya viongozi wake kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Godwin Aiko, Mwenyekiti wa klabu hiyo amesema sababu kubwa ya kuwasimamisha… Read More
  • TAARIFA YA YANGA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUKODISHA TIMU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MUHTASARI WA MKATABA.  1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni iju… Read More

0 comments:

Post a Comment