Supastaa wa Bayern Munich Robert Lewandowski amemshauri Mario Gotze kukataa ofa yoyote Liverpool watakayompa kwa usajili wa majira ya joto
Mcheka na nyavu huyo wa Poland anaamini Gotze anaweza kuthibiti kama moja ya wachezaji bora dunia kama akiendelea kubaki na klabu hiyo ya Bundesliga.
Jurgen Klopp anataka kuungana na mchezaji hyo Liverpool lakini Lewandowski ametoa mtazamo wake juu ya hali hiyo.
Alikiambia Liverpool Echo: “Mario ameonyesha kipindi cha mapumziko ya kimataifa kuwa anaweza kufanya mambo makubwa na ni mchezaji mahiri.
“Hapaswi kufuata kile wasemacho watu kuhusu yeye kwenye magazeti. Hahitaji msukumo wa ziada.
“Hata hivyo Mario anajua kufanya maamuzi ya busara. Tetesi nyingu juu yake ni kero hata hivyo.
“Ni mchezaji wa Bayern na bado ana mechi nyingi mbele yake hadi mwisho wa msimu kuthibitisha ana ubora wa kuichezea Bayern.
“Ana muda wa kutosha kukanusha wanaodai kiwango chake ni dhaifu. Abaki Bayern kwa muda zaidi kwa sababu ni mchezaji bora.”
Wednesday, April 6, 2016
"MARIO GOTZE ATAKUWA MJINGA KWENDA LIVERPOOL"
Related Posts:
STUTTGART 3 ZASHUKA DARAJA MSIMU HUU Msimu wa ligi wa 2015/16 umekuwa msimu mbaya kwa wakazi wa jiji la Stuttgart katika tasnia ya mpira wa miguu. Timu tatu za Stuttgart zimeshuka daraja katika ligi zote 3 zikizoshiriki, Stuttgart iliyokuwa inashiriki… Read More
BAYERN MUCHEN MABINGWA BUNDESLIGA 2015/16 Bayern Muchen wametwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuichapa Ingolstadt kwa jumla ya magoli 2 - 1. Bayern wametwaa ubingwa huo kwa mara ya 27 katika ligi kuu ya Nchini Ujerumani. Magoli yaliyofungwa dakik… Read More
LEWANDOWSKI AIFIKIA REKODI ILIYOWEKWA MIAKA 39 ILIYOPITA MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa sasa Robert Lewandowski amefikia rekodi iliyowekwa miaka 39 iliyopita katika ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundeslig… Read More
PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG AMBWAGA LEWANDOWSKI TUZO ZA MCHEZAJI BORA BUNDESLIGA 2015/16 Mchezaji kandanda bora barani Afrika wa mwaka huu Pierre-Emerick Aubameyang ametawazwa kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mchezaji bora katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga. … Read More
RATIBA EPL LEO JUMAPILI 2 OCTOBER 2016 … Read More
0 comments:
Post a Comment