Vilabu tajiri zaidi duniani vinakutana leo usiku kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, kitu cha kuvutia ni kwamba vilabu vyote hivi vinahitaji kufuzu ili kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
PSG itakuwa mwenyeji wa Manchester City kwenye uwanja wa Parc des Princes huku wakiwa na uchu wa kuitungua klabu nyingine kuoka England na kuitupa nje ya mashindano ya Ulaya baada ya kuifanyia hivyo klabu ya Chelsea kwenye round iliyopita.
City wao waliitupa nje ya mashindano klabu ya Dynamo Kiev kwenye hatua ya 16 cha kupanda na kushuka tangu Pep Guardiola alipotangazwa kukiongoza kikosi hicho kuanzia msimu ujao.
Kikosi cha Manuel Pellegrini kimeporomoka kutoka kuwania ubingwa wa Premier League msimu huu na kwa sasa wanapambana na Manchester United pamoja na West Ham kuwania nafasi nne za juu.
PSG wao tayari wameshatangaza ubingwa wa Ligue 1na hawahofii mechi yao dhidi ya Guingamp siku ya Jumamosi. Miamba hiyo ya jiji la Paris itaingia uwanjani ikiwa na lengo moja tu la kushinda dhidi ya City.
Zlatan Ibrahgimovic ni mshambuliaji ambaye atakuwa akicheza bila ya kuwa na uhakika atakuwa wapi msimu ujao kama ataamua kusalia PSG au la, nyota huyo wa kimataifa wa Sweden bado hajanyanyua taji la ligi ya mabingwa Ulaya.
Laurent Blanc huenda akamkosa Angel Di Maria na Marco Verratti kutokana na majeraha lakini wawili hao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye mechi za Champions League.
City wanaonekana wako vizuri kwa sasa baada ya kuichapa Bournemouth kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya England, lakini Bournemouth imekuwa haipati matokeo mazuri thidi ya klabu kubwa za EPL.
Urejeo wa Kelvin De Bruyne pamoja na Samir Nasri ni habari nzuri kwa City kwasababu kwasababu amekuwa na msaada mkubwa kwenye timu wakati Raheem Starling akiwa miongoni mwa wachezaji watakaoukosa mchezo wa leo
Joe Hart alifanya mazoezi siku ya Jumanne asubuhi na anaweza akarejea uwanjani akitokea majeruhi aliyoyapata kwenye mchezo wa Manchester derby kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa. Yaya Toure hakufanya mazoezi ya pamoja na timu na hatarajiwi kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya PSG.
City itaendelea kucheza bila ya huduma ya Vincent Kompany, huu utakuwa ni mchezo mkubwa kwa Eliaquim Mangala ambaye atakuwa amerejea kwenye ardhi ya nyumbani.
PSG inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo nah ii inatokana na matatizo ya safu ya ulinzi ya Manchester City msimu huu.
0 comments:
Post a Comment