Sunday, March 5, 2017

Samatta atupia mbili Genk ikiua 2 - 1


Jana usiku Mtanzania Mbwana Samatta aliiwezesha timu yake ya KRC GENK kuibuka na ushindi  kwa kupachika goli mbili katika dimba lao la nyumbani la Luminus Arena  katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Club Brugge.

Mbwana Samatta dakika ya 5 alikokota mpira toka katikati ya Uwanja baada ya kupokea pasi toka kwa Malinovsky na kuipa GENK goli la kuongoza kabla ya kufunga la pili akitokea upande wa kushoto baada ya pasi ya Alejandro Pozuelo katika dakika 42, dakika moja badae Brugge walipata goli la kufutia machozi lililofungwa na Izquierdo dakika ya 43.


Matokeo hayo yanaifanya KRC GENK kuendelea kuwa nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wakiwa na point 45,baada ya michezo 29 wakati Club Brugge wao wakiendelea kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 kwa kuwa na jumla ya point 58 sawa na Anderlecht waliyo nafasi ya pili baada ya michezo 29.

0 comments:

Post a Comment